Tanzania, tangu mwaka 2011, mradi ulianzishwa unaotazama kumbukumbu ya kihistoria ya Tanzania kuhusiana na Urithi wa Ukombozi wa Mwafrika. Tasisi husika za umma Tanzania zinajitahidi kulinda na kuhifadhi urithi huo kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho kupitia ufadhili wa UNESCO pamoja na Jumuiya ya Ulaya. Kuna umuhimu mkubwa wa kuruhusu kumbukumbu za uhai wa Nyaraka za Sauti kusikika kupitia nchi husika. Warsha ya kwanza ilifanyika mwaka 2014, TBC, Dar es Salaam. Baada ya miaka mitatu, kabla ya mradi kuisha, warsha nyingine ilifanyika (yakifuatiwa na maonesho). Warsha hiyo ilitoa fursa ya kufunzwa utaalamu wa kidijitali na namna ya kuorodhesha taarifa za nyaraka za sauti. Taasisi nne ziliudhuria mafunzo hayo:Kutoka kulia kwenda kushoto:
Tanzania Broadcast Corporation – TBC : Patricia Makuru, Abdulrazaq Mbena, Neema George, Haruna Sango, Omary Juma Kirimbo & Bethord Mahundi.
National Museum of Tanzania (Kutoka kulia kwenda kushoto: Sophia Fredy, Deusdedith Joseph Kiyumbi & Joyce Nyamfulula)
Records and Archives Management Department of Tanzania (Kutoka kulia kwenda kushoto; Festo Ompeshi & Isabella Robert):
Ministry of Information, Culture Arts and Sports team, in charge of the program ALHP1 African Liberation Heritage Programme (Kutoka kulia kwenda kushoto; Peter Simon & Ingiahedi C. Mduma):
Mwalimu Nyerere Fundation (Edgar Atubonekisye)
Warsha hiyo ilitoa nafasi ya pekee ya mashirikiano na kubadilishana uzoefu wa namna ya kupangilia nyaraka za sauti za kitanzania kwa kufadhiliwa na UNESCO pamoja na Jumuiya ya Ulaya chini ya mradi wa Urithi wa Nyaraka za Kitanzania.
Wakufunzi wa mafunzo hayo walikuwa ni Alexandre Abergel (Muhandisi wa Sauti), na Véronique Ginouvès (CNRS) Mtunza nyaraka. Mafunzo hayo yalisisitiza kuonekana kwa nyaraka za kipekee duniani kupitia mtandao. Ni wakati sahihi sasa kuzitunza nyaraka hizo kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae sababu urithi huu ni tete. Kila siku inayokwenda sehemu muhimu ya nyaraka hizo zinapoteza ubora……timu ya wataalam kutoka taasisi zinazohusika na nyaraka wanafanyakazi ya kukumbusha yaliyopita na kupangilia taarifa zake.
Picha: Warsha TBC, August 2017, Veronique Ginouvès, imepigwa chapa na wakurufunzi, warsha ya tarehe 28th-31st of August 2017, TBC, Dar es Salaam.
English: https://phonotheque.hypotheses.org/22437
Tafsiri: Sophia Fredy.
Inaugural speech of Nancy Kokwenda Kaizilege (UNESCO)
Digitisation with Alexandre Abergel
- Information in french language: http://www.dknews-dz.com/article/84930-tanzanie-prochaine-construction-a-dodoma-dun-centre-du-patrimoine-de-la-liberation-de-lafrique.html [↩]
OpenEdition vous propose de citer ce billet de la manière suivante :
Ceux qui passent à la phonothèque (23 septembre 2017). Kuhuisha nyaraka za sauti Tanzania. Archives de la recherche & Phonothèque. Consulté le 2 novembre 2024 à l’adresse https://doi.org/10.58079/sv9v